1a.
UKIIGAWA dunia katika pande mbili, toka juu hadi chini, Bara la Amerika ni sehemu ya ardhi iliyoko kushoto au magharibi kwako. Huko nyuma eneo hili lilishawahi kujulikana kama Americas au Ardhi Mpya au India Mashariki. Zipo sehemu kuu tatu-Amerika ya Kaskazini [kwenye utajiri zaidi]; Amerika ya Kati au Amerika ya Kilatini[eneo lenye utajiri mdogo na umasikini zaidi]; na Amerika ya Kusini [eneo lenye utajiri wastani lakini masikini ndio wengi zaidi].
Amerika ya Kaskazini ina nchi iliyo chini ya Malkia wa Uingereza iitwayo Canada. Na kuna eneo la Alaska ambalo ni la wenyeji wa asili wa sehemu hiyo lakini sasa linakaliwa na Marekani kutokana na sababu za kiuchumi na mkakati wa kiulinzi.
Mahesabu ya haraka haraka yanaonesha kwamba eneo lote la Amerika ni sawa na asilimia 8.3 ya uso mzima wa dunia; na asilimia 28 ya eneo ambalo ni ardhi duniani.
Idadi ya watu ya eneo zima la Amerika ni kama watu bilioni moja ambao ni asilimia 14 ya idadi ya watu duniani.
Historia ya Bara la Amerika
Hii tunayoijua kama Amerika ilikuwa ni sehemu ya bara kuu la zamani lililoitwa Gondwanaland. Eneo hili lilimeguka kutoka Gondwanaland na kusogezwa pengine kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa wakati huo na hivyo kuunda bara jipya la peke yake. Hii ilikuwa takriban miaka 130 milioni iliyopita. Hata hivyo kipande cha Marekani kuisni kilimeguka peke yake na kile cha Kaskazini peke yake. Miaka kama milioni 15 iliyopita sehemu wazi iliyokuwa kati ya Amerika ya Kusini na Amerika ya Kaskazini iliathriwa na milipuko ya kivolkano iliyosabaisha kuchipuka kwa visiwa kadhaa katika eneo hilo. Udongo wa Amerika za Kaskazini na Kusini pia ulisogezwa baharini na kustawisha visiwa hivyo na huko volkano zikiendelea kuanzisha visiwa vipya. [Hata hivyo, kwa huruma ya Mwenyezi Mungu sehemu hii haiathiriki na Volkano kama sehemu nyingine duniani. Lakini kutokana na kukataa kuwa mstari wa mbele katika kudhibiti uchafuzi wa hali ya hewa duniani hili linaweza kugeuka wakati wowote kutoka sasa].
Hili liliendelea kutokea hadi Amerika ya Kaskazini ikawa imeunganika na Amerika ya Kusini kupitia kile kinachoitwa shingo au kiungo cha Panama.
Kumbuka kwamba eneo kubwa la Gondwanaland lilikuwa ni Afrika.
Kwa hiyo Amerika ya Kusini iliondoka na sehemu ya watu wake na mabara haya yalipoungana watu wa enzi hizo waliweza kuzaana na kusambaa kwenye maeneo mbalimbali ya hizi tunazoziita nchi za Amerika leo. Mathalani kabila linaloitwa 'Inuit' lilipanda mpaka eneo tunaloliita Arctic leo. Hawa walifuatiwa na Mavikingi waliovamia Greenland toka Ulaya kwenye miaka hiyo hiyo.
Huko Greenland na Vinland, hata hivyo, Wavikingi hawakukaa sana wakaondoka kwenye miaka 1500.
Wazungu walianza kutiririka America baada ya Christopher Columbus [1492] kuiona Amerika na kuripoti Ulaya kuwepo kwa ardhi yenye rutuba na eti iliyokuwa ikikaliwa na watu washenzi aliowaita Wahindi Wekundu.
Mauaji ya kimbari na magonjwa mbalimbali yaliyoletwa yalichangia kuwaua wenyeji asili wa Marekani na Waafrika walioletwa kama watumwa kwa maelfu kama sio mamilioni.
Mzungu mmoja anayekubali kuwepo kwa mauaji ya kimbari ni David Stannard .
Kwa kiasi kikubwa serikali nyingi za Ulaya ziliwaunga mkono wahamiaji tokan nchini mwao kwani hili hatimaye lilifanikisha kuwepo na makoloni ya nchi zao barani Amerika.
Sababu kadhaa zilichangia watu kuhama toka Ulaya kwenda Marekani. Sababu hizo ni pamoja na njaa, mateso, dhuluma, kuchoshwa na ukabaila na kunyimwa haki za kibinadamu na vita vya kiimani.
Baadhi ya wahamiaji, hata hivyo, walikuwa ni wezii na malaya waliofukuzwa Ulaya au walijiondokea wenyewe Ulaya ili kubahatisha maisha Amerika.
Wimbi kubwa hata hivyo lilikuwa ni watumwa waliotoroshwa toka Afrika kwenda kuwafanyia wazungu kazi za kuwatajirisha wazungu huko Amerika.
Utumwa huu hadi wa leo umeacha athari kadhaa mbaya za kisaikolojia, kijamii na kiuchumi Afrika. Na athari mojawapo ni ya Waafrika kuwa watu wa kujidhalilisha sana kwa wazungu ikiwemo Wamarekani kama vile wao wenyewe hawana uwezo wa kufanya lolote bila kuwategemea jamaa hawa.
Inaendelea katika 1b.
Saturday, January 12, 2008
Subscribe to:
Posts (Atom)