MAJIBWA wanaugua, kubweka kumepungua,
Mwizi amewanunua, kuiba awatumia,
Kazi yao kutumia, kuzalisha ni nazaa,
Ni wananchi si silaha, na raia si Slaa:
Chama watakiondoa!
Vibaya wanatumia, utusini waingia,
Aibu yawaishia, kinamama walokua,
Na madume nayo pia, kuzomea mazoea,
Ni wananchi si silaha, na raia si Slaa:
Chama watakiondoa!
Na uandishi ukiwa, ndiyo huu umalaya,
Daima naukataa, siingii tasnia,
Kiumbe kujatumia, kma vile changuoa,
Ni wananchi si silaha, na raia si Slaa:
Chama watakiondoa!
Uongo ukweli huwa, na kweli kunajisiwa,
Nyuso zao zinang'aa, fedha wanaposikia,
Na cheo kuahidiwa, japo wengi ni majuha,
Ni wananchi si silaha, na raia si Slaa:
Chama watakiondoa!
Wakubwa wanatambua, benki walizipakua,
Hazina wakazizoa, hata dhahabu kutoa,
Wevi sote tunawajua, wengine wasingiziwa,
Ni wananchi si silaha, na raia si Slaa:
Chama watakiondoa!
Chama chao chahofia, nyuma i ko n yuklia,
CHADEMA ina silaha, bora sana ilokuwa,
Maangamizi walia, yako njiani kutua,
Ni wananchi si silaha, na raia si Slaa:
Chama watakiondoa!
Ila ninawaambia siye atayewaua,
Ndimi zao zachafua, na h asira kututia,
Wananchi tulokuwa, na ukweli twaujua,
Ni wananchi si silaha, na raia si Slaa:
Chama watakiondoa!
Sisi zaidi Slaa, yetu yanavyochochewa,
Wazawa sasa Slaa, fisadi yaelekea,
Bahati haitakuwa, zukunfu kujiokoa,
Ni wananchi si silaha, na raia si Slaa:
Chama watakiondoa!
Wameshindwa kujivua, gamba l ililochakaa,
Mabati wameyatia, kutu yaliyoingia,
Tetenasi twahofia, kila atakayesogea,
Ni wananchi si silaha, na raia si Slaa:
Chama watakiondoa!
Uoza wakumbatia, hadi ndani umejaa,
Chama chanuka balaa, keshokutwa mtajua,
Vijana wanachezewa, na ahadi wamepewa,
Ni wananchi si silaha, na raia si Slaa:
Chama watakiondoa!
Ahadi tuanzojua, za uongo zimekua,
Kila pembe Tanzania, wananchi wanayajutia,
Uoza kuuchagua, uoza kwao hidaya,
Ni wananchi si silaha, na raia si Slaa:
Chama watakiondoa!
Msumari ninatia, uswahiba nauvua,
Ndilo nililoamriwa, na juu aliyekuwa,
Wa dhuluma kukataa, na wasafi kusifia,
Ni wananchi si silaha, na raia si Slaa:
Chama watakiondoa!
Tuesday, March 27, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment