Vyovyote anatumiwa, na wengine
kuwafaa,
Yeye kama chombo huwa, mashinani
kusagiwa,
Mtu kutojitambua, utumwa kwake
tabia!
Hushindwa 'jifikiria, sembuse
kufikiria?
Kama vile ndoo kuwa, au karai
kutumiwa,
Zege akalichangia, pasina na sifa
kuwa,
Mtu kutojitambua, utumwa kwake
tabia!
Dezo atanunuliwa, na walionunuliwa,
Mfukoni akatiwa, ndivyo sivyo
kutumiwa,
Vishilingi akipewa, tajiri
akajisikia,
Mtu kutojitambua, utumwa kwake
tabia!
Kwa cheo huzainiwa, hata wana
kuwaua,
Ukuu akauwania, kwa damu kujimwagia,
Hesabu akijaijua, hubaki kujijutia,
Mtu kutojitambua, utumwa kwake
tabia!
Mara huchanganyikiwa, misuli
kuitanua,
Kisha akaazimia, kuikusanya dunia,
Hajui hatobakia, dunia kumngojea,
Mtu kutojitambua, utumwa kwake
tabia!
Miaka keshahesabia, kisha motoni
kwingia,
Milele kwenda kukaa, kwa anayoyamua,
Laiti angetambua, vivyo asingetumiwa,
Mtu kutojitambua, utumwa kwake
tabia!
Roho inapotolewa, ndio ukweli hujua,
Tena sana akalia, dakika kuruhusiwa,
Mema akachangia, moto kwenda
ukimbia,
Mtu kutojitambua, utumwa kwake
tabia!
Rushwa hutaka kutoa, malaika kugawia,
Wapate kumuachia, dakika akasalia,
Ila hatohurumiwa, macho akayakodoa,
Mtu kutojitambua, utumwa kwake
tabia!
No comments:
Post a Comment