KATIKA
yetu maisha, nasibu tunapangiwa,
Hauwezi
kukatisha, wala kujiongezea,
Kadari
huitimisha, liandikwalo likawa,
Kuoa
umpendaye, huwa ni bahati kubwa !
Joto
wanaotupasha, na werevu kudhania,
Mioyo
wakatingisha, na vifua kuinya,
Sio
tunaoozeshwa, bahati huwakimbia,
Kuoa
umpendaye, huwa ni bahati kubwa !
Wasiotukorofisha,
na presha kututia,
Daima
wasiobisha, na uume kujitia,
Na
wasiokutingisha, hadi ukachanganyikiwa,
Kuoa
umpendaye, huwa ni bahati kubwa !
Pingu
wanaotuvisha, moyoni hawakuingia,
Ila
muda ulitosha, kipindi kikafatia,
Ubishi
unapoisha, miaka kuikimbia,
Kuoa
umpendaye, huwa ni bahati kubwa !
Wengine
tuanozeshwa, kama vile twaolewa,
Ya
wake kuyawezesha, yasipate kufifia,
Na
ndugu wakikorofisha, ukajikuta pabaya,
Kuoa
umpendaye, huwa ni bahati kubwa !
Kuna
wengine wazusha, mimba kukusingizia,
Wenye
nazo wamechoshwa, wala hawakuridhia,
Si
mtu wa kubisha, jukumu ukachukua,
Kuoa
umpendaye, huwa ni bahati kubwa !
Kunazo
zisizo kesha, za mkeka twaambiwa,
Ulipojiburudisha,
puani yakakutokea,
Kwao
alishawachosha, mwanya wakiungojea,
Kuoa
umpendaye, huwa ni bahati kubwa !
Kuna
za kujiimarisha, kipato kikatulia,
Wa
mkwasi kumkosha, hata sura akipwaya,
Unatafuta
maisha, mengine yatafatia,
Kuoa
umpendaye, huwa ni bahati kubwa !
Kuna
wengine angusha, ujinga umewajaa,
Ila
wajua zungusha, wanatia ukichaa,
Mkiyaanza
masiha, hujiona umeliwa,
Kuoa
umpendaye, huwa ni bahati kubwa !
Kuna
wa kuburudisha, si wa kukuongezea,
Kwalo
hilo linatosha, kazi hapo yaishia,
Ukitaka
jumlisha, kuzidisha na kutoa,
Kuoa
umpendaye, huwa ni bahati kubwa !
Kuna
wa kubabaisha, jiko lipo kujitia,
Heshima
kutokuisha, japo unaning'inia,
Na
mikasa ya maisha, ndani huwa yabakia,
Kuoa
umpendaye, huwa ni bahati kubwa !
Kuna
wa kuelimisha kitu wasichokijua,
Ni
wabishi wa kuchosha, hadi wanapoumia,
Hapo
wakijirekebisha, jema waweza ambua,
Kuoa
umpendaye, huwa ni bahati kubwa !
Kuna
wa kuneemesha, utajiri mkajua,
Mkayapenda
maisha, na baraka kujaliwa,
Kama
ni kuyarefusha, dua mkajiombea,
Kuoa
umpendaye, huwa ni bahati kubwa !
Kuna
ya kukinaisha, nyumba ikawa balaa,
Ukataka
yakomesha, katikati kuishia,
Ila
ukajikausha, majukumu kutimia,
Kuoa
umpendaye, huwa ni bahati kubwa !
Katika
yetu maisha, ndoa nyingi ni sanaa,
Twajaribu
kuchekesha, na kukimbia udhia,
Tunatania
watasha, ukweli kutokujua,
Kuoa
umpendaye, huwa ni bahati kubwa !
Na
DNA rabsha, siri inazifichua,
Katikati
ya maisha, watu wakajichukia,
Walodhani
wajitosha, wakakuta wapungua,
Kuoa
umpendaye, huwa ni bahati kubwa !
No comments:
Post a Comment