YAO kutoingilia, ni busara
inakuwa,
Katika hii dunia, ndugu ni
kuwaachia,
Yao wanayatambua, kwa dira na
historia,
Ndugu wanapogombana, chukua jembe
kalime!
Huna la kukadiria, katikati
kuingia,
Udhia utajiria, pamwe aibu na
haya,
Ila wakishatulia, 'siache
wasalimia,
Ndugu wanapopatana, chukua kapu
kavune!
Matusi yakitembea, na magumi
kutambaa,
Nyumbani kwako ingia, jembe
kwenda kuchukua,
Ujihimu kwelekea, shambani
kujilimia,
Ndugu wanapogombana, chukua jembe
kalime!
Kununa kukikiishia, tabasamu
wakatoa,
Wakawa wakumbatia, kile
walichochukia,
Kapu wende kutungua, kivuno
kitakujia,
Ndugu wanapopatana, chukua kapu
kavune!
Ngebe zinapotambaa, na mateke
kutembea,
Inuka ulipokaa, kiserema
kuchukua,
Matembele kuwania, uende
kupalilia,
Ndugu wanapogombana, chukua jembe
kalime!
Kicheko wakiangua, na hafla
kuisikia,
Usiache karibia, na hodi
kujigongea,
Sahau ikishaingia, huwa raha na
furaha,
Ndugu wanapopatana, chukua kapu
kavune!
Mbwa wakikubwekea, mguu ukate
njia,
Mlango kutouvaa, usije ukavuliwa,
Yako ukakimbilia, hadi uishe
wasaa,
Ndugu wanapogombana, chukua jembe
kalime!
Nyimbo ukizikia, kama vile
wamelewa,
Milango hufunguliwa, yote wazi
inakuwa,
Ndani weza kuingia,nawe upate
tanua,
Ndugu wanapopatana, chukua kapu
kavune!
Bunduki ukisikia, usiwe
wachungulia,
Waweza kutunguliwa, dirishani
ukikaa,
Mvunguni kiingia, usalama wanunua,
Ndugu wanapogombana, chukua jembe
kalime!
Sherehe zikikolea, na mapambo
yakajaa,
Jua yameamuliwa, na wewe
kujititimua,
Kapu kutokuachia, tupu
halitarejea,
Ndugu wanapopatana, chukua kapu
kavune!
No comments:
Post a Comment