Wawili wanaopendana, wakaacha
aminiana,
Wivu ukagandamana, na hofu ya
kuumizana,
Hufariki muamana, iwe kama ni laana,
Wajapokuchukizana, wapenzi huchukiana!
Huisha kuaminiana, watu
wakahofiana,
Ikawa ni kuwindana, kwa usiku na
mchana,
Raha wakawa hawana, ila ya
kuchunguana,
Wajapokuchukizana, wapenzi
huchukiana!
Zama waliokipatana, wakawa si
waelewana,
Shere wameshachezana, mashavu
wanuniana,
Na mioyo inapindana, ubaya
kutakiana,
Wajapokuchukizana, wapenzi
huchukiana!
Mahaba walopeana, sumu
wakamwagiana,
Na nje kukashifiana,ya ndani
kufichuana,
Siri pakawa hakuna, kila kitu ni
bayana,
Wajapokuchukizana, wapenzi
huchukiana!
Haya watatenguana, na udhu
kukatazana,
Mbio wakatimuana, kwenda
wasikotakikana,
Dunia ikawaona, sio watu wa
maana,
Wajapokuchukizana, wapenzi
huchukiana!
Sura watachafuana, zikawa tambo
hazina,
Soni zikawa ni suna, paisna
kuhifadhiana,
Wchache wakulingana, katu
kutotokezana,
Wajapokuchukizana, wapenzi
huchukiana!
Dira huharibiana, ziishe
kupindana,
Mbele sasa kutoona, wawe
wanaangaliana,
Huruma wakawa hana, na utu
waozeana,
Wajapokuchukizana, wapenzi
huchukiana!
Wakawa wa kushindana, ubaya
kufanyiana,
Muafaka kuzozana, waaswapo
kupatana,
Lengo wakawa hawana, wakabaki
madubwana,
Wajapokuchukizana, wapenzi
huchukiana!
Binadamu muungwana, haya
anapoisana,
Na huruma kutona, kwa marefu na
mapana,
Vingine ya binti suna, hayawani
humuona,
Wajapokuchukizana, wapenzi
huchukiana!
No comments:
Post a Comment