AIMA nitakumbuka, nilizopiga hatua,
Nikitamani
kukushika, neno nikakuambia,
Bali
nyuma nilivutika, nawe ukatangulia,
Pendo
lisilochipua, moyoni linabakia !
Msingi
tulipofika, japo nilikutania,
Midomo
nikaishika, kupapasa nikajua,
Matokeo
yalipotoka, sote hatukwendelea,
Pendo
lisilochipua, moyoni linabakia !
Baada
tu ya mwaka, nawe ukajaingia,
Mtaa
juu ulitoka, wa chini nikaanzia,
Mwendowe
nikaudaka, usingizini nikiwa,
Pendo
lisilochipua, moyoni linabakia !
Na
kila nilipotaka, jambo langu kukwambia,
Ulimi
ulifyatuka, salamu tu kuitoa,
Machowe
yaliniteka, hadi nguvu kuishiwa,
Pendo
lisilochipua, moyoni linabakia !
Miaka
ikafutika, umbali ukaingia,
Hadi
niliposumbuka, na hadithi kuambiwa,
Dar
umebahatika, kazi unajifanyia,
Pendo
lisilochipua, moyoni linabakia !
Sikuwa
nayo haraka, hadi nilipochelewa,
Na
mara nilipofika, mbele ulishatangulia,
Machoni
ukanitoka, urulaini kwenda kuwa,
Pendo
lisilochipua, moyoni linabakia !
Ajabu
haya mashaka, hayakunipa ukiwa,
Bure
sikutaabika, zaidi ningelilia,
Letu
halikuandikwa, na wala lisingekuwa,
Pendo
lisilochipua, moyoni linabakia !
Ila
ninayo hakika, moyoni unachanua,
Jinalo
siachi tamka, na wengine kugawia,
Mtu
akiliitika, naona unarejea,
Pendo
lisilochipua, moyoni linabakia !
Hautorudi
hakika, hilo ninalitambua,
Ila
siku itafika, na mimi nikiingia,
Kwanza
nitalolitaka, wapi wakaa kujua,
Pendo
lisilochipua, moyoni linabakia !
Kama
inaruhusika, wewe nitakuchagua,
Mkono
nikakushika, ukirimba kulilia,
Wengine
sintowataka, ila wewe maridhia,
Pendo
lisilochipua, moyoni linabakia !
No comments:
Post a Comment