Mengi yamehadithiwa, na mifano
kutolewa,
Vipande vya historia, darasa
mkajaliwa,
Ni vito vilivyokuwa, kinyesini
vyafukiwa,
Yamo kwenye mashairi, ila nani
anasoma ?
Akili waliojaa, viini wajimwagia,
Kubaini wafulia, sio
waliochaguliwa,
Neema ya kubabia, huishi kuiogea,
Yamo kwenye mashairi, nani wa
kutafakari ?
Maandishi hutokea, bali
hutojisomea,
Akili zikakwambia, wewe sana
unajua,
Hadi unakoelekea, njia zako
kufungiwa,
Yamo kwenye mashairi, ila nani
anasoma ?
Ulidhani wasikiwa, watu viziwi
wakawa,
Ulidhani wayajua, ukakuta
hayakuwa,
Bishara zikakwambia, njia
umeshapotea,
Yamo kwenye mashairi, nani wa
kutafakari ?
Zama zilizoishia, mawazo
yalifukiwa,
Leo yanachimbuliwa, mengi watu
wanajua,
Vitendo wakumbukia, awali
vilivyokuwa,
Yamo kwenye mashairi, ila nani
anasoma ?
Mizani waichukua, kisha
wakaangalia,
Kama sawa imekuwa, au vitu
imetiwa,
Kila inapopwelea, kelele
utasikia,
Yamo kwenye mashairi, nani wa
kutafakari ?
Maji yamewazidia, waogopa
angamia,
Bahari nchi kavu kuwa,kwao taabu
itakuwa,
Bado hawajatembea, majini
wakaelea,
Yamo kwenye mashairi, ila nani
anasoma ?
Neema zimesambaa, ja senene na
mvua,
Yawashinda magunia, wapi kwingine
kukaa,
Na kumbikumbi wazaa, si muda
watatokea,
Yamo kwenye mashairi, nani wa
kutafakari ?
Isije kuwa balaa, ikawa kizaazaa,
Kasi itapopungua, mwendo rudi
nyuma ukawa,
Na ari ikaishia, moshini
kuyoyomea,
Yamo kwenye mashairi, ila nani
anasoma ?
Tabia naihofia, dhrau iliyojaa,
Hoja inayonyanyapaa, bila asili
kujua,
Mioyo kukangamaa, kama kaukau
zikawa,
Yamo kwenye mashairi, nani wa
kutafakari ?
No comments:
Post a Comment