Tuesday, February 14, 2012

C H A M A


Chama kisicho na watu, masikini walokuwa,

Kikageuzwa mstiu, wa tajiri na nguvadoa,

Watu wakawa viatu, kubasi za kuogea,

Huwa chacheza upatu, uhai kuuchezea,

Watu wakishakijua,

Haraka watakivua,

Mbali kukimbilia,

Salama ilipokuwa,

Ya kheri kuambulia,

Kwa shari kuihofia,

Chamacho kujabakia,

Na mapumba nazo chuya,

Dawa inayotakiwa, wanyonge kuwanyanyua,

Chamani wakaingia, na kufunzwa yanayofaa,

Asili kuzingatia, Alutta kuendelea,

Yote yakafikiriwa, chama kujizaa upya,

Nyoyo zipate tulia, kazi moja kubakia,

Mabadiliko kuzua, na madhubuti kikawa,

Ushindi kutabiriwa, na watu kukubaliwa,

Chama budi kuchagua, tajiri au fakiri !

No comments: