Chema huwa chajiuza
Kibaya chajitembeza
Marashi hupakwa uoza
Kilicho frshi wakapuuza
Hii ni dunia
Wanayajua
Wakiamua
Shari ikiwa
Kufukuzia
Ubani kutia
La kuvunda likanukia
Na wengi kulparamia
Kipindi lisilochukua
Likanuka tena kwa udhia!
Chama
Chama kinachochanganyikiwa
Ni gunia lililotuna kwa upupu kujaa
Ndani viongozi wote sio wa kutulia
Ukubwa huanza mapema kukimbilia
Wakasahau ya hao waliowachagua
Na kuyaganga tu yale yanayowadfaa
Ubinafsi hujaa
Uroho na tamaa
Ukubwa wa njaa
Jeta hajaujua
Mikopo kutwaa
Wengine kuvaa
Na ahadi kutoa
Kiti wakitwaa
Deni wataua
Wakijafulia
Balaa huzua
Wizi na njaa
Nchi ikavia
Ndiko ambako sasa tayari twaelekea
Makelele mmeanza wanachama kusikia
Kama ni mimi karata ningelitunukiwa
Wengine pembeni mapema wangesogea
Kofiani kuchagua hata nisiowatambua
Denda likaishilia na mbali kutokomea!
Monday, February 6, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment