Friday, February 10, 2012

Chama cha wezi kikiwa

{ Chama kikitekwa nyara na wezi/}

Afrika nawaambia, vya wezi kuvihofia,
Si vyama vya kuenziwa, kwenye nchi huwa baa,
Watu wakahadaiwa, hata roho kuzitoa,
Chama cha wezi kombora, lisilokuwa na dira,
Huenda njia kugura, nyuma likajasowera,
Lianze tena kufura, kuilipua hadhira,
Kila pembe huchakura, watu wakagaragara,
Wakubwa wakishapora,
Wadogo humalizia!

Magazeti hutumiwa, nchi huku yaibiwa,
Waandishi walokuwa, kama malaya wakawa,
Fedha wakishazipewa raia kutowatetea,
Chama cha wezi kombora, lisilokuwa na dira,
Huenda njia kugura, nyuma likajasowera,
Lianze tena kufura, kuilipua hadhira,
Kila pembe huchakura, watu wakagaragara,
Wakubwa wakishapora,
Wadogo humalizia!

Televisheni zapewa, matangazo ya bandia,
Roho yasiyojaliwa, ila ni kuzainiwa,
Malengo kuyafikia, ya hazina kuibiwa,
Chama cha wezi kombora, lisilokuwa na dira,
Huenda njia kugura, nyuma likajasowera,
Lianze tena kufura, kuilipua hadhira,
Kila pembe huchakura, watu wakagaragara,
Wakubwa wakishapora,
Wadogo humalizia!

Mbal walishaanzia, hadi mfumo kwingia,
Vyama vingi vajikwaa, wananchi sio shujaa,
Ukweli hawajajua, kudanganywa waendelea,
Chama cha wezi kombora, lisilokuwa na dira,
Huenda njia kugura, nyuma likajasowera,
Lianze tena kufura, kuilipua hadhira,
Kila pembe huchakura, watu wakagaragara,
Wakubwa wakishapora,
Wadogo humalizia!

Bado wanayadhania, yalokuwa ujamaa,
Kumbe ubepari njia, ndiyo iliyokubaliwa,
Wao ni histora, kumbe hawajajitambua,
Chama cha wezi kombora, lisilokuwa na dira,
Huenda njia kugura, nyuma likajasowera,
Lianze tena kufura, kuilipua hadhira,
Kila pembe huchakura, watu wakagaragara,
Wakubwa wakishapora,
Wadogo humalizia!

Fedha walituibia, mashirika kuchukua,
Ya umma yakazaliwa, na mikononi kuwafia,
Kisha wakajiuzia, shilingi hatukupewa,
Chama cha wezi kombora, lisilokuwa na dira,
Huenda njia kugura, nyuma likajasowera,
Lianze tena kufura, kuilipua hadhira,
Kila pembe huchakura, watu wakagaragara,
Wakubwa wakishapora,
Wadogo humalizia!

Ushirika waliua, maendeleo kuvia,
Leo yatima twalia, hapana pa kukimbilia,
Hii ndiyo asilia, Mwafrika kajaliwa,
Chama cha wezi kombora, lisilokuwa na dira,
Huenda njia kugura, nyuma likajasowera,
Lianze tena kufura, kuilipua hadhira,
Kila pembe huchakura, watu wakagaragara,
Wakubwa wakishapora,
Wadogo humalizia!

Nyumba wamezichukua, wenyewe kujigawia,
Ardhi waikamia, wageni kuwapatia,
Na dhahabu wametoa, wageni kuwagawia,
Chama cha wezi kombora, lisilokuwa na dira,
Huenda njia kugura, nyuma likajasowera,
Lianze tena kufura, kuilipua hadhira,
Kila pembe huchakura, watu wakagaragara,
Wakubwa wakishapora,
Wadogo humalizia!

Ufisadi yaridhia, nchi imefagiliwa,
Hazna nyeupe kuwa, na sisi tunashangaa,
Na wakubwa walokuwa, matajiri wamekua,
Chama cha wezi kombora, lisilokuwa na dira,
Huenda njia kugura, nyuma likajasowera,
Lianze tena kufura, kuilipua hadhira,
Kila pembe huchakura, watu wakagaragara,
Wakubwa wakishapora,
Wadogo humalizia!

Uchamungu twaishia, ndio maana twaliwa,
Na Mola kutuhurumia, anaona ni kinyaa,
Budi kumgeukia, hawa kuwashughulikia,
Chama cha wezi kombora, lisilokuwa na dira,
Huenda njia kugura, nyuma likajasowera,
Lianze tena kufura, kuilipua hadhira,
Kila pembe huchakura, watu wakagaragara,
Wakubwa wakishapora,
Wadogo humalizia!

Asili haikuwa, uwizi hatukulea,
Afrika ilikuwa, daima yaukataa,
Mwiz hakuhurumiwa, aliingizwa hatia,
Chama cha wezi kombora, lisilokuwa na dira,
Huenda njia kugura, nyuma likajasowera,
Lianze tena kufura, kuilipua hadhira,
Kila pembe huchakura, watu wakagaragara,
Wakubwa wakishapora,
Wadogo humalizia!

Wezi tunawavumilia, hali yetu yawa mbaya,
Wepesi kusimulia, hadithi zisizokuwa,
Maneno kuyajengea, sijaona, haijawa,
Chama cha wezi kombora, lisilokuwa na dira,
Huenda njia kugura, nyuma likajasowera,
Lianze tena kufura, kuilipua hadhira,
Kila pembe huchakura, watu wakagaragara,
Wakubwa wakishapora,
Wadogo humalizia!

Februari 11, 2012
Dar es salaam.

No comments: