HIVI sasa saa ngapi ?
Nawe umeenda wapi?
Rudi
Njoo
Sasa
Nipo
Peke
Raha
Sina
Wahi ninakungojea
Mkononi uje chanua
Na harufu kuiridhiya
Nitakayo kupumua, sauti ya kusikiya, nyororo ya kutomasa na kizuri cha kuangalia na kukigusa
Ni saa
Kukaa
wawili
Azizi
Pumzi
Kutua
Maisha kuendelea, kupata na kutumia, kupewa na kupokea, kuenzi na kuenziwa, kupenda na ukapendwa
Kawaida ikarejea!!!
Sasa ni saa ngapi ?
No comments:
Post a Comment