Mola amewajalia, wazee kuwagawia,
Hekima za kuenziwa, na wengine kutumia,
Na busara nazo pia, si haba hazijapungua,
Wa hekima na busara, nyie msipowatumia,
Wengine watawataka,
Wajinga mkabakia,
Na kuja kuyajutia,
Laiti tungelijua !
Kama ukishalijua, hili ukazingatia,
Akili walojaliwa, ni wachache walokuwa,
Wanangoja kufikiwa, ushauri kuutoa
Wa hekima na busara, nyie msipowatumia,
Wengine watawataka,
Wajinga mkabakia,
Na kuja kuyajutia,
Laiti tungelijua !
Kizazi twakishangaa, leo kilichokuwa,
Kinaona kinajua, hata wasiyoyajua,
Na hata wakiyajua, vigumu kuyaelewa,
Wa hekima na busara, nyie msipowatumia,
Wengine watawataka,
Wajinga mkabakia,
Na kuja kuyajutia,
Laiti tungelijua !
Kauli wanazotoa, moto zazidi chochea,
Udugu zinauua, kwa petroli kumwaa,
Na amani wafumua, kuchanika itakuwa,
Wa hekima na busara, nyie msipowatumia,
Wengine watawataka,
Wajinga mkabakia,
Na kuja kuyajutia,
Laiti tungelijua !
Wazee walojaliwa, daima wadharauliwa,
Waonekana kinyaa, vigumu kuwaingia,
Au uchoyo umejaa, na kubwa iliyo njaa,
Wa hekima na busara, nyie msipowatumia,
Wengine watawataka,
Wajinga mkabakia,
Na kuja kuyajutia,
Laiti tungelijua !
Au uchoyo umejaa, na kubwa iliyo njaa,
Chakula kilichokua, wengine kuwagawia,
Matumbo yawazuzua, mkenge wanaingia,
Wa hekima na busara, nyie msipowatumia,
Wengine watawataka,
Wajinga mkabakia,
Na kuja kuyajutia,
Laiti tungelijua !
Kucha asiyejaliwa, kujikuna huugua,
Wenyewe wanaojilia, na dhiki hujaachiwa,
Pekee wakabakia, hata nyumba ikiungua,
Wa hekima na busara, nyie msipowatumia,
Wengine watawataka,
Wajinga mkabakia,
Na kuja kuyajutia,
Laiti tungelijua !
Hasemi mwenye kujua, macho kwake kubabia,
Ya kwao huwaachia, wenyewe kujishikia,
Nafasi ikitokea, ukweli ataugawa,
Wa hekima na busara, nyie msipowatumia,
Wengine watawataka,
Wajinga mkabakia,
Na kuja kuyajutia,
Laiti tungelijua !
Uchi mtu kujakua, njiani anatembea,
Huku yeye adhania, eti nguo amevaa,
Akija kushtukia, watu wanamzomea,
Wa hekima na busara, nyie msipowatumia,
Wengine watawataka,
Wajinga mkabakia,
Na kuja kuyajutia,
Laiti tungelijua !
Yameanza kutokea, bado yataendelea,
Sisi si wa kuzomea, ila mengine twajua,
Vigelegele ni ngoa, wambeya twawaachia,
Wa hekima na busara, nyie msipowatumia,
Wengine watawataka,
Wajinga mkabakia,
Na kuja kuyajutia,
Laiti tungelijua !
Februari 11, 2012
Dar es salaam.
Saturday, February 11, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment