Na mini nakuambia, yako ninahifadhia,
Isipokuwa yalokuwa, nje ya uwezo kuwa,
Siachi kukusetiri, na mini nisetiriwa:
Ila ya wabaya wako, watu lazima kujua,
Hadi radhi kuitoa,
Wakupe na msamaha!
Yako nitakufichia, wengine kutoyajua,
Ila nje uliyotoa, siwezi kuyazuia,
Aibu yako ikawa, mimi haukunambia,
Siachi kukusetiri, na mini nisetiriwa:
Ila ya wabaya wako, watu lazima kujua,
Hadi radhi kuitoa,
Wakupe na msamaha!
Vya watu ulivyotwaa, kurudisha watakiwa,
Laana kutoachiwa, wana wasio hatia,
Mama mpenda familia, hagtotaka kuumia,
Siachi kukusetiri, na mini nisetiriwa:
Ila ya wabaya wako, watu lazima kujua,
Hadi radhi kuitoa,
Wakupe na msamaha!
Watoto unatakiwa, kheri wapate zawadiwa,
Mama kutokuingia, kwenye maovu ya dunia,
Mwenyezi kumrudia, tawba hataoikataa,
Siachi kukusetiri, na mini nisetiriwa:
Ila ya wabaya wako, watu lazima kujua,
Hadi radhi kuitoa,
Wakupe na msamaha!
Shetani alokwingia, pengine atamtoa,
Kawaida kurejea, ibilisi kumwambaa,
Na zako hawa jamaa, salama wakatunukiwa,
Siachi kukusetiri, na mini nisetiriwa:
Ila ya wabaya wako, watu lazima kujua,
Hadi radhi kuitoa,
Wakupe na msamaha!
Nami ninakuombea, tobayo kukubaliwa,
Na rehema ukapewa, na msamaha maridhawa,
Ukaijali familia, pamoja tukarejea,
Siachi kukusetiri, na mini nisetiriwa:
Ila ya wabaya wako, watu lazima kujua,
Hadi radhi kuitoa,
Wakupe na msamaha!
No comments:
Post a Comment