Ujana maji ya moto, hayakawii kupoa,
Waendao maliwato, kuwahi wanatakiwa,
Ukichelewa kwa ndoto, baridi utaogea,
Ujana maji ya moto, hayachelewi kupoa!
Hushikwa na mchecheto, baridi kuyaogea,
Huwa hayana mvuto, japo yanasisimua,
Hunawa kwa manukato, wale wanaozidiwa,
Ujana maji ya moto, hayachelewi kupoa!
Watu huwapiga ngoto, na wengine kuumia,
Mambo yake mtokoto, tabia hukengeua,
Jazba yao mseto, kila kitu huchukia,
Ujana maji ya moto, hayachelewi kupoa!
Wengine huota kwato, kama farasi wakawa,
Ikawacheza fukuto, mbegu ovyo kupandia,
Lakini wawe wazito, ya kwao kuja kulea,
Ujana maji ya moto, hayachelewi kupoa!
Watazipanda kokoto, wategemee maua,
Huu mkubwa mchoto, vigumu kuuchukua,
Hubakia kama ndoto, na kweli haitokuwa,
Ujana maji ya moto, hayachelewi kupoa!
Mambo budi mchakato, kupanga na kupangua,
Haya ukiwa mzito, mbele hutoendelea,
Na maisha si mvuto, ni kutunza na kulea,
Ujana maji ya moto, hayachelewi kupoa!
Ujana maji ya moto, hayakawii kupoa,
Waendao maliwato, kuwahi wanatakiwa,
Ukichelewa kwa ndoto, baridi utaogea,
Ujana maji ya moto, hayachelewi kupoa!
Hushikwa na mchecheto, baridi kuyaogea,
Huwa hayana mvuto, japo yanasisimua,
Hunawa kwa manukato, wale wanaozidiwa,
Ujana maji ya moto, hayachelewi kupoa!
Watu huwapiga ngoto, na wengine kuumia,
Mambo yake mtokoto, tabia hukengeua,
Jazba yao mseto, kila kitu huchukia,
Ujana maji ya moto, hayachelewi kupoa!
Wengine huota kwato, kama farasi wakawa,
Ikawacheza fukuto, mbegu ovyo kupandia,
Lakini wawe wazito, ya kwao kuja kulea,
Ujana maji ya moto, hayachelewi kupoa!
Watazipanda kokoto, wategemee maua,
Huu mkubwa mchoto, vigumu kuuchukua,
Hubakia kama ndoto, na kweli haitokuwa,
Ujana maji ya moto, hayachelewi kupoa!
Mambo budi mchakato, kupanga na kupangua,
Haya ukiwa mzito, mbele hutoendelea,
Na maisha si mvuto, ni kutunza na kulea,
Ujana maji ya moto, hayachelewi kupoa!
No comments:
Post a Comment