Monday, February 13, 2012

viogozi wetu lena,

Viongozi wetu hawa,
Kazini ajifunzia,
Miko wnaikataa,
Shule bora ingekuwa,
Na wanayoyaamua,
Nchi inadidimia,
Kisa hawajkijua,
Ujuzi umepungua,
Kila mtu ajitia,
Kila kitu anajua,
Mwishowasiku huwa,
Yale yasiyojijua,
Viongozi wetulena, wapaswa kujitambua,
Chuoni wakarejea, miundombinu kujengewa,
Uongozi kutambua, ni kuingiz sio kutumia,
Na ndipo hapo hakika, nchi upya kuzaliwa,
Tanzania kutovia, nyambizi kuendelea

Kona zote tunajua,
Watu wazidi fulia,
Na juu waliokuwa,
Wasaii yasokuwa,
Sakafu twaifukua,
Na kuta tunazibomoa,
Linavuja nalo paa,
Bado tunaangalia,
Utenzi usiokuwa,
Nani kughani radhia?
Na kinachoendelea,
Waigizaji tumekua,
Viongozi wetulena, wapaswa kujitambua,
Chuoni wakarejea, miundombinu kujengewa,
Uongozi kutambua, ni kuingiz sio kutumia,
Na ndipo hapo hakika, nchi upya kuzaliwa,
Tanzania kutovia, nyambizi kuendelea

Uongo tukitumia,
Wenyewe utaturudia,
Kwa kiapo kuapia,
Kwa biblia kunyanyu,
Na Kurani kutumia,
Itabaki kuchechewa,
Maruweruwe yakawa,
Watu wasiojiua,
Hubaki kusahauliwa,
Chini wakishafukiwa,
Mchanga wakageukia,
Majina yakapotea,
Viongozi wetulena, wapaswa kujitambua,
Chuoni wakarejea, miundombinu kujengewa,
Uongozi kutambua, ni kuingiz sio kutumia,
Na ndipo hapo hakika, nchi upya kuzaliwa,
Tanzania kutovia, nyambizi kuendelea

Nchi tataka ridhaa,
Maarifa na ulua,
Mengi ya kujipangia,
Na mengine kufumua,
Yawe ya kujisukia,
Kisha ya kuyazuia,
Kwa imani kutambua,
Na Mola kumuhofia,
Vinginevyo ikiwa,
Ni nazaa na balaa,
Mola asiporidhia,
Kila kitu hupotea,
Viongozi wetulena, wapaswa kujitambua,
Chuoni wakarejea, miundombinu kujengewa,
Uongozi kutambua, ni kuingiz sio kutumia,
Na ndipo hapo hakika, nchi upya kuzaliwa,
Tanzania kutovia, nyambizi kuendelea

No comments: