Nchi budi kujaliwa,
Vyama safi vilokuwa,
Wizi visivyoujua,
Wala haramu kutwaa,
Mola anavyojalia,
Na viranja kuwafaa:
Demokrasia Zambia, nchi inayojijua,
Ushindani unakua, na uchumi wakomaa,
Sio kama Tanzania, tunguli twategemea,
Na misaada kuwazia, hata isipotakiwa,
Demokrasia hukua, watu wanapojijua,
Lazima kujitambua, na mchango wa kutoa,
Ukishaijua nia, hujua na yko njia,
Mkwaza demokrasia, maendeleo huvia:
Yafaa kumzuia,
Kiongozi kutokua,
Udikteta kuzaa,
Nchi utakaochafua,
Watu waje kuumia,
Na nuksi na balaa,
Kwa tunayoyahofia,
Ya kweli yakaja kuwa!
Viongozi hujaliwa,
Safi sana walokuwa,
Katu wasiodhamiria,
Mali kuja jilimbia,
Na ukubwa kuutumia,
Kama silaha ya mabaya:
Demokrasia Zambia, nchi inayojijua,
Ushindani unakua, na uchumi wakomaa,
Sio kama Tanzania, tunguli twategemea,
Na misaada kuwazia, hata isipotakiwa,
Demokrasia hukua, watu wanapojijua,
Lazima kujitambua, na mchango wa kutoa,
Ukishaijua nia, hujua na yko njia,
Mkwaza demokrasia, maendeleo huvia:
Yafaa kumzuia,
Kiongozi kutokua,
Udikteta kuzaa,
Nchi utakaochafua,
Watu waje kuumia,
Na nuksi na balaa,
Kwa tunayoyahofia,
Ya kweli yakaja kuwa!
Hofu inayowajaa,
Kwa usawa kuzingatia,
Daima kutotulia,
Kuona kazi lafanyiwa,
Wanyonge kuwasaidia,
Kila wanapozidiwa:
Demokrasia Zambia, nchi inayojijua,
Ushindani unakua, na uchumi wakomaa,
Sio kama Tanzania, tunguli twategemea,
Na misaada kuwazia, hata isipotakiwa,
Demokrasia hukua, watu wanapojijua,
Lazima kujitambua, na mchango wa kutoa,
Ukishaijua nia, hujua na yko njia,
Mkwaza demokrasia, maendeleo huvia:
Yafaa kumzuia,
Kiongozi kutokua,
Udikteta kuzaa,
Nchi utakaochafua,
Watu waje kuumia,
Na nuksi na balaa,
Kwa tunayoyahofia,
Ya kweli yakaja kuwa!
Haki wasionunua,
Wala kujakujiuzia,
Dhaifu huangalia,
Wasije kudhulumiwa,
Udhibiti huzingatia,
Kila muda kila saa:
Demokrasia Zambia, nchi inayojijua,
Ushindani unakua, na uchumi wakomaa,
Sio kama Tanzania, tunguli twategemea,
Na misaada kuwazia, hata isipotakiwa,
Demokrasia hukua, watu wanapojijua,
Lazima kujitambua, na mchango wa kutoa,
Ukishaijua nia, hujua na yko njia,
Mkwaza demokrasia, maendeleo huvia:
Yafaa kumzuia,
Kiongozi kutokua,
Udikteta kuzaa,
Nchi utakaochafua,
Watu waje kuumia,
Na nuksi na balaa,
Kwa tunayoyahofia,
Ya kweli yakaja kuwa!
Kariakoo bidhaa,
Viwanja wanaonunua,
Wajane kuwaibia,
Na vizee kuvibabua,
Hili watalikataa,
Mitaani wakijua:
Demokrasia Zambia, nchi inayojijua,
Ushindani unakua, na uchumi wakomaa,
Sio kama Tanzania, tunguli twategemea,
Na misaada kuwazia, hata isipotakiwa,
Demokrasia hukua, watu wanapojijua,
Lazima kujitambua, na mchango wa kutoa,
Ukishaijua nia, hujua na yko njia,
Mkwaza demokrasia, maendeleo huvia:
Yafaa kumzuia,
Kiongozi kutokua,
Udikteta kuzaa,
Nchi utakaochafua,
Watu waje kuumia,
Na nuksi na balaa,
Kwa tunayoyahofia,
Ya kweli yakaja kuwa!
Uchumi huunyanyua,
Kwa raia kutumia,
Sio kwa kutegemea
Matepeli walokuwa,
Nje wanaotokea,
Watu wema kujitia:
Demokrasia Zambia, nchi inayojijua,
Ushindani unakua, na uchumi wakomaa,
Sio kama Tanzania, tunguli twategemea,
Na misaada kuwazia, hata isipotakiwa,
Demokrasia hukua, watu wanapojijua,
Lazima kujitambua, na mchango wa kutoa,
Ukishaijua nia, hujua na yko njia,
Mkwaza demokrasia, maendeleo huvia:
Yafaa kumzuia,
Kiongozi kutokua,
Udikteta kuzaa,
Nchi utakaochafua,
Watu waje kuumia,
Na nuksi na balaa,
Kwa tunayoyahofia,
Ya kweli yakaja kuwa!
Husaidia sanaa,
Bei nzuri kujipatia,
Wasanii wakang'aa,
Na maisha kujifaa,
Hofu ikawapotea,
Wakabaki kuendelea:
Demokrasia Zambia, nchi inayojijua,
Ushindani unakua, na uchumi wakomaa,
Sio kama Tanzania, tunguli twategemea,
Na misaada kuwazia, hata isipotakiwa,
Demokrasia hukua, watu wanapojijua,
Lazima kujitambua, na mchango wa kutoa,
Ukishaijua nia, hujua na yko njia,
Mkwaza demokrasia, maendeleo huvia:
Yafaa kumzuia,
Kiongozi kutokua,
Udikteta kuzaa,
Nchi utakaochafua,
Watu waje kuumia,
Na nuksi na balaa,
Kwa tunayoyahofia,
Ya kweli yakaja kuwa!
Michezo huangalia,
Walimu kuwaachia,
Makocha wakaachiwa,
Yao wanayoyajua,
Mwisho matokeo kuwa,
Kipimo cha kuwafaa:
Demokrasia Zambia, nchi inayojijua,
Ushindani unakua, na uchumi wakomaa,
Sio kama Tanzania, tunguli twategemea,
Na misaada kuwazia, hata isipotakiwa,
Demokrasia hukua, watu wanapojijua,
Lazima kujitambua, na mchango wa kutoa,
Ukishaijua nia, hujua na yko njia,
Mkwaza demokrasia, maendeleo huvia:
Yafaa kumzuia,
Kiongozi kutokua,
Udikteta kuzaa,
Nchi utakaochafua,
Watu waje kuumia,
Na nuksi na balaa,
Kwa tunayoyahofia,
Ya kweli yakaja kuwa!
Ushindani huibua,
Kila sekta kuingia,
Watu kujashindania,
Kuwa bora Tanzania,
Medali wakachukua,
Na ndarahima nazo pia:
Demokrasia Zambia, nchi inayojijua,
Ushindani unakua, na uchumi wakomaa,
Sio kama Tanzania, tunguli twategemea,
Na misaada kuwazia, hata isipotakiwa,
Demokrasia hukua, watu wanapojijua,
Lazima kujitambua, na mchango wa kutoa,
Ukishaijua nia, hujua na yko njia,
Mkwaza demokrasia, maendeleo huvia:
Yafaa kumzuia,
Kiongozi kutokua,
Udikteta kuzaa,
Nchi utakaochafua,
Watu waje kuumia,
Na nuksi na balaa,
Kwa tunayoyahofia,
Ya kweli yakaja kuwa!
Amani itachanua,
Kwa vitendo vya radhia,
Raia wakaazimia,
Kitu kimoja wakawa,
Adui kutoingia,
Kati ya ndugu na jamaa:
Demokrasia Zambia, nchi inayojijua,
Ushindani unakua, na uchumi wakomaa,
Sio kama Tanzania, tunguli twategemea,
Na misaada kuwazia, hata isipotakiwa,
Demokrasia hukua, watu wanapojijua,
Lazima kujitambua, na mchango wa kutoa,
Ukishaijua nia, hujua na yko njia,
Mkwaza demokrasia, maendeleo huvia:
Yafaa kumzuia,
Kiongozi kutokua,
Udikteta kuzaa,
Nchi utakaochafua,
Watu waje kuumia,
Na nuksi na balaa,
Kwa tunayoyahofia,
Ya kweli yakaja kuwa!
Umoja ukajilea,
Sio kwa kushinikiziwa,
Ikawa ndiyo tabia,
Hasidi wakaishiwa,
Waache kuja tuvaa,
Mabaya kutuletea:
Demokrasia Zambia, nchi inayojijua,
Ushindani unakua, na uchumi wakomaa,
Sio kama Tanzania, tunguli twategemea,
Na misaada kuwazia, hata isipotakiwa,
Demokrasia hukua, watu wanapojijua,
Lazima kujitambua, na mchango wa kutoa,
Ukishaijua nia, hujua na yko njia,
Mkwaza demokrasia, maendeleo huvia:
Yafaa kumzuia,
Kiongozi kutokua,
Udikteta kuzaa,
Nchi utakaochafua,
Watu waje kuumia,
Na nuksi na balaa,
Kwa tunayoyahofia,
Ya kweli yakaja kuwa!
Uongo huukataa,
Ukweli ukaenea,
Pasiwe wa kutumia,
kama choo alokuwa,
Ukisha jimalizia,
Hakuna kuwaangalia:
Demokrasia Zambia, nchi inayojijua,
Ushindani unakua, na uchumi wakomaa,
Sio kama Tanzania, tunguli twategemea,
Na misaada kuwazia, hata isipotakiwa,
Demokrasia hukua, watu wanapojijua,
Lazima kujitambua, na mchango wa kutoa,
Ukishaijua nia, hujua na yko njia,
Mkwaza demokrasia, maendeleo huvia:
Yafaa kumzuia,
Kiongozi kutokua,
Udikteta kuzaa,
Nchi utakaochafua,
Watu waje kuumia,
Na nuksi na balaa,
Kwa tunayoyahofia,
Ya kweli yakaja kuwa!
Jamii huinyanyua,
Ujuzi ukaenea,
Mengi wakajifanyia,
Bila nje kutegemea,
Wavumbuzi kuvumbua,
Vyote vinavyotufaa:
Demokrasia Zambia, nchi inayojijua,
Ushindani unakua, na uchumi wakomaa,
Sio kama Tanzania, tunguli twategemea,
Na misaada kuwazia, hata isipotakiwa,
Demokrasia hukua, watu wanapojijua,
Lazima kujitambua, na mchango wa kutoa,
Ukishaijua nia, hujua na yko njia,
Mkwaza demokrasia, maendeleo huvia:
Yafaa kumzuia,
Kiongozi kutokua,
Udikteta kuzaa,
Nchi utakaochafua,
Watu waje kuumia,
Na nuksi na balaa,
Kwa tunayoyahofia,
Ya kweli yakaja kuwa!
Hukua teknolojia,
Na wanaoitumia,
Nchi namba kushikilia,
Juu sana kujakuwa,
Na mengine kugundua,
Wenzetu wakatumia:
Demokrasia Zambia, nchi inayojijua,
Ushindani unakua, na uchumi wakomaa,
Sio kama Tanzania, tunguli twategemea,
Na misaada kuwazia, hata isipotakiwa,
Demokrasia hukua, watu wanapojijua,
Lazima kujitambua, na mchango wa kutoa,
Ukishaijua nia, hujua na yko njia,
Mkwaza demokrasia, maendeleo huvia:
Yafaa kumzuia,
Kiongozi kutokua,
Udikteta kuzaa,
Nchi utakaochafua,
Watu waje kuumia,
Na nuksi na balaa,
Kwa tunayoyahofia,
Ya kweli yakaja kuwa!
Utamaduni hukua,
Yakalindwa manufaa,
Pasiwe wa kutuchezea,
Asili yetu kujua,
Na lugha kuitumia,
Kiswahili kikakua:
Demokrasia Zambia, nchi inayojijua,
Ushindani unakua, na uchumi wakomaa,
Sio kama Tanzania, tunguli twategemea,
Na misaada kuwazia, hata isipotakiwa,
Demokrasia hukua, watu wanapojijua,
Lazima kujitambua, na mchango wa kutoa,
Ukishaijua nia, hujua na yko njia,
Mkwaza demokrasia, maendeleo huvia:
Yafaa kumzuia,
Kiongozi kutokua,
Udikteta kuzaa,
Nchi utakaochafua,
Watu waje kuumia,
Na nuksi na balaa,
Kwa tunayoyahofia,
Ya kweli yakaja kuwa!
Monday, February 13, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment